November 21, 2018


Nahodha wa timu ya Taifa ya Uganda inayoshiriki michuano ya Dar Copa Dar es Salaam Beach Soccer, Kibirige Meddie amewapa mbinu wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kufanikiwa kufuzu Afcon.

Stars wapo kundi L ambalo ni timu ya Uganda tu imefanikiwa kufuzu huku Lesotho na  Capeverde matumaini yao ni mpaka Machi mwakani kwenye mechi za mwisho walizobakiwa nazo mkononi.


Meddie amesema kuwa Stars wana nafasi ya kufuzu endapo watafanikiwa kushinda dhidi ya Uganda ila wanatakiwa wajipange kwa kuwa sio kitu chepesi kama wanavyofikiria.


"Mpira una kanuni zake hivyo kwa Stars kuweza kufuzu wanatakiwa wafanya kazi kubwa kwenye maandalizi na watumie vema uwanja wa nyumbani, rekodi hazidanganyi hasa unapozungumzia timu ya Uganda, wakijituma watafanikiwa kupata matokeo," alisema.


Uganda wamefuzu baada ya kufikisha pointi 13, Lesotho wana pointi 5 sawa na Tanzania huku Cape Verde wakiwa na pointi 4 wote wana nafasi ya kufuzu endapo watajipanga vizuri mechi zao za marudio.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic