November 2, 2018


Ofisa habari wa timu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa kwa sasa wamewekeza nguvu kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa uwanja wa Manungu, Morogoro.

Bwire bado ana kumbukumbu za kufungwa bao 5-0 dhidi ya Simba katika mchezo wao uliochezwa jumapili amesema kuwa haikuwa mpango wa Mungu kuwapapasa Simba, hivyo wanakwenda kuwapapasa Mtibwa Sugar.


"Tupo vizuri, kikosi chetu ni cha ushindani morali ya wachezaji imeongezeka hivyo tunakwenda tukiwa tunajua tunataka kuchukua pointi tatu ugenini mbele ya Mtibwa.


"Tunauwezo wa kufanya makubwa, kufungwa haimaanishi hatuwezi, hivyo Mtibwa wajiandae kisaikolojia kupapaswa square maana hamna namna tumejipanga," alisema Bwire.


Mara ya mwisho Ruvu Shooting walipokutana na Mtibwa Sugar msimu uliopita kwenye Uwanja wa Manungu, Ruvu Shooting walishinda kwa mabao 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic