MBELGIJI SIMBA ATAJA HATMA YA NIYONZIMA NDANI YA KIKOSI CHAKE
Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Mbelgiji, Patrick Aussema ameibuka na kukanusha uvumi ulionezwa mitandao kuwa mchezaji wake, Mrwanda, Haruna Niyonzima atandoka ndani ya timu hiyo.
Mbelgiji huyo ameibuka na kueleza hayo baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Nyasa Bullets ya Malawi uliomalizika kwa suluhu tasa ya bila kufungana.
Aussems amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote akieleza bado anahitaji huduma ya kiungo huyo ambaye amemuelezea kuwa kiwango chake kinazidi kuimarika.
Niyonzima alipangwa na Aussems katika mchezo na Nyasa ambapo alikuwa kwenye kikosi cha kwanza na baada ya kumalizika kwa mechi hiyo Mbelgiji alieleza kufurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo.
Simba imekipiga na timu hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi yake ya kimataifa dhidi ya Mbabane Swallows ya Ligi ya Mabingwa Afrika.








0 COMMENTS:
Post a Comment