November 5, 2018


Na George Mganga

Mwanachama wa Yanga, Edgar Chibula ameibuka na kumshangaa Katibu Mkuu wa Matawi ya klabu hiyo, Boaz Kupilika juu ya kupinga matamko ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuhusiana na suala la kufanya uchaguzi.

Chibula amepinga maelezo ya Kupilika ambaye alisema BMT hawana mamlaka ya kuwapangia kipi cha kufanya ikiwemo uchaguzi wao kusimamiwa na Kamati ya Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Mwanachama huyo ameeleza kuwa ifikie hatua Yanga ikubali matokeo na badala yake ifanye uchaguzi kwa kuwa imekuwa ikiendeshwa bila ya kuwa na watu muhimu.

Yanga imesimama kwa muda bila ya kuwa na Mwenyekiti wa klabu, na baadaye Wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji walijiondoa pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga.

Jambo limasukuma Chibula na akitaka ifikie hatua Yanga inapaswa kuwa imara kwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi hico kwa mujibu wa katiba ya klabu.

1 COMMENTS:

  1. Edgar unaijua katiba ya yanga?wao wanapaswa kuishauri yanga na kuwa waangalizi tu si vinginevyo yanga wote tunataka uchaguzi hakuna asiyetaka ila kwa mujibu wa katiba yetu tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic