Mshambuliaji wa Coastal Unioon ambaye pia ni mdhamini wa timu hiyo Ali Kiba amekuwa akisugua benchi kwa muda mrefu tangu asajiliwe na kikosi hicho cha Tanga.
Katika michezo 13 ambayo Coastal Union wamecheza yeye amecheza mchezo mmoja tu dhidi ya Kagera Sugar akitokea benchi dakika ya 89.
Kocha Mkuu wa Coastal Union Juma Mgunda amesema kuwa Kiba ni moja kati ya wachezaji waliosajiliwa kuitumikia timu hiyo hivyo atapata nafasi kadri siku zinavyokwenda.
"Kiba ni mchezaji wa Coastal na tuna wachezaji wengi ambao tumewasajili hivyo kucheza kwake inategemea na majukumu ambayo tunakabiliana nayo," alisema.








0 COMMENTS:
Post a Comment