November 3, 2018


Na George Mganga

Beki wa kushoto wa klabu ya Simba, Mohammed Hussein, amefunguka na kuzungumzia namna alivyopata tabu juzi wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Kwa mujibu wa Radion kupitia Spoti Leo, Hussein maarufu kwa jina la Tshabalala, amesema kuwa wachezaji waliomsumbua zaidi ni Shiza Kichuya na Aishi Manula ambao aliwaelezea kuwa ni hatari zaidi kwenye sekta hiyo.

Kichuya na Manula walionekana kuongoza zaidi mashambulizi ya kummwagia maji na michanga Hussein kisha kulichafua pia gari lake kwa matope.

Hata hivyo, Hussein ameeleza kuwa analichukulia tukio hilo kama faraja kwake akiamini ni upendo walionao wachezaji wenzake pamoja na ushirikiano ndani ya timu.

Wakati Hussein akielezea hayo, Simba leo inashuka dimbani kucheza na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic