Kocha Mkuu wa timu ya Ndanda FC, Malale Hamsini amesema kuwa katika dirisha dogo anahitaji kusajili wachezaji wanne tu ili aweze kuongeza nguvu.
Hamsini amesema kuwa wamekuwa na mwendo wa kobe kwenye ligi kwa kuwa hawana wachezaji wenye uzoefu katika ligi hivyo anajipanga kuangalia uwezekano wa kuwasajili wachezaji wenye uzoefu.
"Wachezaji wangu wengi hawana uzoefu kwenye ligi hivyo nakijenga kikosi katika mazingira magumu, kwenye dirisha dogo nina mpango wa kuweza kuongeza wachezaji wanne ili kuongeza nguvu ya ushindani," alisema.
Ndanda wamecheza michezo 13 na kufanikiwa kushinda 3 huku wakipoteza michezo 6, sare 4 na mbili kati ya hizo ni dhidi ya vigogo Simba na Yanga.








0 COMMENTS:
Post a Comment