WALIOSABABISHA MKUTANO MKUU YANGA KUPIGWA KALENDA WATAJWA
Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kusogeza mbele mkutano wao mkuu wa dharua uliokuwa umepangwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu.
Ratiba ya kusogezwa mbele kwa mkutano huo ni kutokana na timu ya klabu hiyo kuwa na mechi kadhaa za Ligi Kuu Bara.
Badala sasa ya kufanyika Novemba 24, mkutano huo umepangwa kuwepo tarehe 1 Disemba huku mahala ikiwa haijajulikana itakuwa wapi.
Yanga itakuwa na mechi mbili kuelekea mwezi wa 12 ambapo itakuwa inacheza dhidi ya Mwadui FC Novemba 22. huko CCM Kambarage Shinyanga na baadaye dhidi ya Kagera Sugar Novemba 25.
Uongozi umewataka wanachama wa klabu hiyo kutulia hivi sasa na baadaye utakuja kuwajuza ni wapi mkutano huo utafanyika.








Jinga kweli...rudia kichws cha habari halafu ujiulize kama kweli umeelezea waliosababisha!
ReplyDeleteWacha kutuzingua ww ah kichwa cha habari hakifanani kabisa nauliyoyaeleza
ReplyDeleteKichwa cha habari hakiendani na habari ulio iandika kwa hiyo inatakiwa
ReplyDeleteHuyu jamaa tutamkimbia na li-blog lake hili. Anaelezea vitu ambavyo haviwiani kabisa na title! mbali na hilo, hawa jamaa zake wanaahirisha mkutano kisa mechi! Mbona Simba ilicheza Mkwakwani na JKT Tanzania wakati huku Dar unafanyika Mkutano wa uchaguzi Mkuu?.
ReplyDelete