November 8, 2018


Na George Mganga

Baada ya aliyekuwa mchezaji wao, Obrey Chirwa kusajiliwa na Azam FC, uongozi wa klabu ya Yanga umeibuka na kueleza kuwa wao wanafanya usajili kwa mapendekezo ya Kocha, imeelezwa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, ameeleza kuwa Yanga inafanya usajili kwa mahitaji ya Mwalimu hivyo si sahihi kusajili tu ilimradi.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Chirwa kusajiliwa Azam wakati ikielezwa Yanga ndiyo walifanya mpango wa kumtumia tiketi ya ndege Mzambia huyo lakini wakapigwa kete na Azam.

Ilielezwa kuwa Yanga walimrejesha Chirwa ili waje wamalizane naye lakini mambo yamekuwa tofauti kama ambayo ilikuwa imepangwa mwanzo.

Tayari Chirwa ametambulishwa leo na uongozi wa Azam FC na ataanza rasmi kuitumikia kuanzia Nover=mba 15 ambapo dirisha dogo litakuwa limeshafunguliwa.

6 COMMENTS:

  1. muongo wewe mwandishi nakumbuka kuwa zahera alimkataa na ulilipoti sasa imekuwa bao tena kweli bongo bangla

    ReplyDelete
  2. Yaani ulichokiripoti mwenyewe mara umekisahau, duuuh huu uandishi bado sijaufahamu vizuri. Ulisema Zahera kamkataa Chirwa, leo Azam waipiga bao Yanga. Ungesema baada ya Zahera kumkataa Chirwa, Azam wameamua kumchukua, simple as that!!

    ReplyDelete
  3. Na ulitoa picha Chirwa akiwa uwanja wa Taifa kushuhudia mechi mojawapo ya Yanga, ukadai Zahera kamkataa mchezaji huyo. Leo suala la bao limetoka wapi? Kumbuka wewe unachema wa nini, mwenzako anasema atampata lini? Hata kwa Ngoma mlisema sena, Azam wamemtibu na sasa anaanza kutoa matunda kwa kufunga mabao ya muhimu kwenye timu yake.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakumbushia tu, siku hiyo Chirwa akiwa uwanjani, Yanga walikuwa wakicheza na timu ya Alliance FC. Hawa waandishi wanazi hawa! Kweli cku hizi kazi hazifanywi kwa kipawa, bali zinafanywa baada ya kukosa kazi fulani. Hajui kazi hii haihitaji unazi!.

      Delete
  4. Ngoma hajatibiwa na Azam, walimpa tu muda wa kupumzika akiwa Yannaga alikuwa anazuga huyo! Dhambi yake itamtafuna, kuchukua fedha za Club na kusingizia ugonjwa, achene hizo.

    ReplyDelete
  5. Ngoma alipelekwa Afrika Kusini ndugu..............Haaaaaa unazi upo wapi?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic