November 8, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka wapenzi na wanachama wake kuwa na subira kwa imejipanga kufanya usajili wa maana dirisha dogo, imeelezwa.

Yanga imeamua kuvunja ukimya kutokana na kuanza kupokea malalamiko juu ya viwango vya baadhi ya wachezaji wake ambao inawategemea kwa sasa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amesema kuwa kwa sasa uongozi unajipanga kuhakikisha inakuja kufanya usajili pindi dirisha likapofunguliwa.

Hatua hii imekuja mara baada ya wanayanga kadhaa kuwatupia lawama wachezaji ikiwemo Heritier Makambo ambaye wameanza kumuona kama ana mapungufu uwanjani.

Dirisha la usajili litafunguliwa Novemba 15 mwezi huu na tayari baadhi ya timu zimeshaanza kuingia mikataba ya awali ikiwemo Azam FC baada ya kumalizana na Obrey Chirwa aliyewahi kuichezea Yanga.

5 COMMENTS:

  1. Makambo mara hii amekuwa hafai? Si alikuwa Makambo, mabao?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  2. Makambo mchezaji wa magazetini. Huyo mimi nilipomuona kwa mara ya kwanza tu niligundua hamna kitu!

    ReplyDelete
  3. Duuu! Hawa jamaa! Sasa ni mchezaji gani kwao ni mzuri wakati kila siku "vice msemaji" wao anatuambia kuwa wana kikosi kipana na chenye wachezaji wazuri?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga ina kikosi kizuri sana tu ila kwenye striking force kunahitajika kuongezewa nguvu. Na Makambo anatakiwa awe anatokea bench. Kuwe na mchezaji anayeanza mwenye uwezo mkubwa kuliko yeye

      Delete
  4. Nafikiri sorting yao haikufanyika vizuri kwa Makambo. Ila Yanga wana kikosi imara sana akina Shishimbi, Kamusoko, Ngasa, Martin, Raphael, Amis Tambwe na Ajib mbona wote wapo vizuri tu!!!!!!!!!!

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic