November 3, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kutokuwepo uwanjani kwa nyota kama Kelvin Yondani na Paul Godfrey 'Boxer' hakumpi hofu kwa kuwa wapo wenye uwezo wa kuchukua nafasi zao kesho watakapocheza na Ndanda FC, uwanja wa Taifa.

Yondani ataukosa mchezo huo kwa kuwa anasumbuliwa na maumivu ya goti ambayo aliyapata katika mchezo uliopita dhidi ya Lipuli FC, Boxer alipata kadi nyekundu kwenye mchezo huo.

"Wachezaji ambao hawatakuwepo kuna mbadala wao ambao watachukua nafasi zao kucheza, ninawaamini wachezaji wangu najua watanipa matokeo mazuri kwani hicho ndicho nimewaambia wafanye mapema kabisa.

"Vincent Andrew 'Dante' atachukua nafasi ya Yondani kwa kuwa ameshapona majeraha yake ya misuli na kumaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu, nafasi ya Paul itachukuliwa na Juma Abdul," alisema.

Yanga na Ndanda zimekutana mara nane tangu Ndanda ipande daraja msimu wa 2013/14 ambapo Yanga wameshinda mara nne huku Ndada wakishinda mara moja na wametoa sare michezo mitatu.

2 COMMENTS:

  1. Ingekuwa kuongea ni mabao mbona ungekuwa unapiga hamsa mkono

    ReplyDelete
  2. Moira hauchezwi mdomoni...na ukikutana na Simba tena ni kichapo tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic