Baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwafungia wasanii wa muziki kutoka lebo ya Wasafi Diamond na Rayvan pamoja na kufuta kibali cha kufanya Tamasha la Wasafi Festival kwa muda usiojulikana wameamua kuomba radhi kwa kosa lao walilofanya la kukiuka maagizo ya BASATA.
Diamond amesema kuwa wanakosea kwa kuwa ni binadamu hali ambayo inawafanya waombe msamaha kwa BASATA, Wizara ya Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni pamoja na watu wote waliokwazika.
"Kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba radhi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, BASATA, Wizara ya Michezo, Habari, Sanaa na Utamaduni pamoja na wote waliokwazika kwa 'kuperfom' wimbo wa Mwanza ambao tulizuiliwa kuutumia katika shoo yetu ya Wasafi Festival, Mwanza.
"Tumekosea 'kuperfom' wimbo ambao ulifungiwa japo tulijitahidi kuweza kufuata maadili ya kazi ili kuwa vijana bora katika Taifa letu, tunaawasa mashabiki na wasanii wenzetu kuwa mabalozi wazuri wa tamaduni zetu kupitia sanaa," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment