Mashabiki wa Yanga wameonyesha wanachotaka ni timu yao kuendelea kutoa vichapo.
Walithibitisha hilo baada ya kutembeza mchango wa papo kwa hapo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha, jana wakati Yanga ikiivaa African Lyon.
Katika mechi hiyo ambayo Yanga walishinda kwa bao 1-0, mashabiki hao walipita jukwaani wakichangisha mchango huo katika ndoo ya plastiki.
Mashabiki wengi walionekana kukubaliana na kuchanga kuanzia Sh 1,000 na kuendelea.
Yanga ipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara ikiw ana pointi 47 baada ya kucheza mechi 17 na haijapoteza mechi hata moja.
Pamoja na mwendo huo mzuri katika Ligi Kuu Bara, Yanga imekuwa ikielezwa kutokuwa vizuri kifedha na wachezaji wake wamekuwa wakichelewa kulipwa mishahara yao lakini wamekuwa wakionyesha juhudi kwa kuendelea kujituma.
0 COMMENTS:
Post a Comment