December 9, 2018






Michael Aonga ni mshindi wa droo ya 66 wa promosheni inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa ijulikanayo kama Shinda Zaidi na SportPesa ambapo kwa watumiaji wa mitandao yote ya simu yaani Airtel, Zantel, Tigo, Vodacom pamoja na Halotel wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kama bajaji, simu janja(smartphone), jezi orijino ya Simba na Yanga pamoja na ticketi ya kushuhudia mechi za ligi ya msimu 2018/2019 za Ligi Kuu England na ile ya Hispania maarufu kama La Liga.


Wakati wa makabidhiani ya bajaji Michael alisema hakuamini kama ameshinda bajaj kweli mpaka alipoiiona timu ya SportPesa imefika nyumbani kwake ndio furaha yake ya ushindi ilikamika.

Akizungumza na timu ya ushindi Aonga alisema anashukuru kuona ubashiri wake na SportPesa kwa shilingi 1000 tu  na umempa mafaniko ya kushinda bajaj ambayo anaamini itamsaidia kujiimarisha kiuchumi.


"Kupitia bajaj hii sasa ntaweza kulipa kodi ya nyumba kwa wakati hii ilikuwa ni zaidi ya changamoto kwangu mbali ya hilo ntajitahidi kununua mashine ya kisasa ya kufyatulia tofali maana kazi yangu mimi ni fundi ujenzi." alisema Aonga.

Aidha, Aonga anaamini huu ndio wakati wa yeye kuitwa bosi na kuheshimiwa na jamii inayomzunguka maana atakuwa amempa ajira dereva atakayeendesha bajaj yake.


"Leo nimeamini ule usemi usemao lala maskini amka ukiwa tajiri, SportPesa imeniamsha na Utajiri hivi unafikiri na usawa huu tulionao kumiliki bajaj ni kitu cha mchezo hili sio jambo dogo ni kubwa sana lazima niwashukuru sana na hakika sitoacha kucheza, kwanza ni kampuni iliyo ya kweli na hawana longolongo kwenye kulipa pesa mara unapoweka ubashiri uliosahihi, mechi zikiisha tu fedha ulizoshinda zinawekwa kwenye akaunti yako papo hapo," aliongeza  Aonga.


Kubashiri na SportPesa ni kwa kila Mtanzania mwenye umri juu ya miaka 18 ambapo  kupitia simu yako ya mkononi iwe ya tochi au simu janja unachotakiwa kufanya ni kupiga *150*87# na kisha Weka pesa namba ya kampuni ni 150888 na kumbukumbu namba ni 888 baada  ya hapo sasa unaweza weka ubashiri wako kwenye michezo mbalimbali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic