Kocha mkuu wa timu ya Yanga ambaye ni kocha bora wa mwezi Novemba amesema kuwa hana hofu kukutana na Biashara United leo kutiokana na nafasi ambayo inashika kwa sasa.
Biashara United imepanda daraja msimu huu
haijawa na mwenendo mzuri kwa kuwa wamecheza michezo14 na kufanikiwa kushinda
mchezo mmoja wakiwa nafasi ya 20.
Zahera amesema kuna ugumu mkubwa wa kucheza na timu ambayo ipo nafasi ya chini kwenye msimamo, anatambua kwa kuwa alikutana na ugumu kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya
Tanzania Prisons.
"Tulicheza na Prisons, nadhani wengi waliona
mazingira tuliyopitia na ushindani ulivyokuwa hivyo nimewaambia wachezaji wangu
wanakutana na timu ngumu wanapaswa nao wawe wagumu.
"Kitu kikubwa ambacho tunafikiria ni kupata
poitnt tatu na haziwezi kuja hivihivi mpaka tupambane, ili tuweze kupata
matokeo, mashabiki waendelee kutupa sapoti," alisema.
Kwenye mchezo wa leo utakaochezwa saa moja uwanja
wa Taifa wachezaji kama Ibrahimu Ajibu ana matatizo ya kifamilia na Mrisho Ngasa ana adhabu ya kadi nyekundu wataukosa mchezo .
0 COMMENTS:
Post a Comment