December 8, 2018


Mshambuliaji  wa timu ya Simba, raia wa Rwanda Meddie Kagere, anatambua kuwa mchezo wao unaofuata kimataifa ni dhidi ya Nkana FC, hali iliyomfanya kujiandaa kuja na mtindo mpya kwa ajili ya kushangilia pindi akifunga bao.


Kagere ambaye kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ana mabao 2 aliyowafunga nje ndani Mbabane Swalows ya Eswatin alianza kutumia staili mpya ya kufumba macho yote mawili akiwa  Dar es Salaam na alipowafunga akiwa Eswatini alianza kuchezesha mikono yote miwili.


Kagere amesema kuwa hana staili moja ya kushangilia anazo nyingi tu kichwani mwake anazitumia kutokana na aina ya matukio na namna anavyofanikiwa kufunga bao.

"Mpira una mambo mengi hivyo sioni taabu kubadilisha staili yangu ya ushangiliaji nikiwa ndani ya uwanja hasa baada ya kushinda kwani hicho ni kitu ambacho kinatokea chenyewe tu bila kupanga.


"Kuziba jicho ama kuziba macho ni mpira tu na aina ya ushangiliaji ambayo nipo nayo hivyo baada ya kufunga mechi zangu za kimataifa najiandaa kuja na aina mpya tutakaposhinda katika mchezo wetu ujao wa kimataifa," alisema.


Simba inatarajiwa kuvaana na Nkana FC ambayo anachezea Mtanzania Hassan Kessy Desemba 14 mwaka huu nchini Zambia na marudiano yatakuwa Desemba 21 mwaka huu katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic