Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans van Der Pluijm, amefunguka kuwa ndoto yake ni kuipa timu yake ubingwa wa ligi kuu msimu huu na hilo litawezekana kutokana na juhudi yao wanayoifanya kwenye kila mchezo.
Azam ambayo maskani yake ni mitaa ya Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar, haijapoteza mchezo wowote wa Ligu Kuu Bara hadi sasa ikiwa tayari imeshuka dimbani mara 15 na kujikusanyia pointi 39, baada ya kushinda michezo 12 na kutoka sare kwenye michezo mitatu.
Hans amesema kuwa kutwaa taji la ligi kuu msimu huu ndiyo ndoto yao kubwa na watafanikiwa kufanya hivyo kutokana na jinsi wachezaji wake wanavyopambana kwenye kila mchezo, huku akiweka wazi kuwa nidhamu ya wachezaji na kujituma kwa asilimia 100 ndiyo kitu pekee kitakachompa ubingwa msimu huu.
“Ubingwa ndiyo ndoto kubwa tuliyonayo na tutahakikisha tunacheza kwa nidhamu mara zote na kwenye kila mechi tutacheza kama fainali pasipo kukata tamaa, kwa sababu kila timu ambayo inakutana na sisi hucheza kwa kujituma zaidi ili iweze kupata matokeo lakini hilo halitaweza kutuzuia kuwa mabingwa,” alisema Hans.
Haya maneno aliyasema hata wakati yuko Singida utd.
ReplyDelete