December 29, 2018


Hatimaye Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga amekubali kukutana na wachezaji wa zamani wa timu hiyo kwa ajili ya kusuluhisha masuala mbalimbali yakiwemo ya wachezaji na viongozi.

Wachezaji hao wakiongozwa na Ramadhan Kampira hivi karibuni walituma maombi kwa Zahera wakimuomba wakutane wakae ili kuweza kuweka mambo sawa haswa kuhusiana na Kamati ya Usajili pamoja na suala la Beno Kakolanya.

Kuhusu Kamati ya usajili, wachezaji wamelenga kumalizana na Zahera kwa kuwaombea msamaha viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Idara hiyo, Hussein Nyika juu ya kudanganya ripoti ya usajili wa wachezaji katika dirisha dogo.

Aidha, wachezaji hao wamepanga kumshawishi Zahera amsamehe Beno Kakolanya ili aweze kurejea kikosini na aendelee na majukumu yake kama kawaida kwakuwa Kakolanya bado ni sehemu ya wachezaji Yanga.

Mkongomani huyo amekubali wito huo na amesema atamalizana nao atakapopata muda kwakuwa hivi sasa yupo jijini Mbeya na kikosi kwa ajili ya kibarua cha Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City.

4 COMMENTS:

  1. Uwezo wa kufikiri na ukosefu wa weledi linaweza kuwa tatizo kubwa katika ukuzaji soka letu. Inawezekana nia ya wachezaji wa zamani ikawa njema lakini pia inawezekana wakawa wanatumika pasipo kujijua. Vema kabla hawajakutana na Zahera wakajiuliza je soka linahitaji nidhamu ya aina gani? Je ubabaishaji na ulaghai una nafasi gani katika soka? Je wachezaji watalipwa mishahara yao wanayodai lini? Je ilisipolipwa Kakolanya hatagoma tena? Je Kakolanya hatokuwa kirusi baada ya kurejeshwa kundini? Wakipata majibu hayo tusubiri matokeo

    ReplyDelete
  2. Yanga imekuwa timu ya kibabaishaji sana, Nyika na wenzako wekeni mapato na matumizi hadharani, timu ambayo ilipata millioni 950 sportpesa, 600 CAF, ada za wanachama, Azam na viingilio lakini bado tunaambiwa inaukata?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah kwa hesabu ya haraka hiyo ni 1.5 bilioni.Kuna umuhimu wa kujua mchanganuo maana sidhani usajili wa wachezaji ulifika 300 million

      Delete
  3. wanaopinga uchaguzi ndio haohao wanaofaidika na yanga sasa hivi hakuna wa kuhojiwa kwa sababu timu haina viongozi wanaoeleweka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic