December 20, 2018



Kocha wa Timu ya Lipuli, Seleman Matola na mchezaji wa Zamani wa Simba, amesema kuwa Simba wana nafasi nzuri ya kupata matokeo mbele ya wapinzani wao Nkana FC katika mchezo wa Ligi kuu ya Mabingwa Afrika utakaochezwa uwanja wa Taifa, Jumapili.

Simba wanahitaji ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa marudio baada ya kupoteza mchezo wa kwanza waliocheza nchini Zambia kwa kufungwa mabao 2-1 wakiwa ugenini.

"Uwezo mkubwa kwa wachezaji wa Simba endapo wataamua kuutumia ili kupata matokeo wanaweza kupindua matokeo hasa wakiamua kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani ni kanuni tu na nidhamu, wanapaswa wajiamini na wapambane kutafuta matokeo," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic