Mchezo wa Ligi Kuu unaendela leo kati ya African Lyon na Yanga uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Abdallah Shaibu 'Ninja' anawanyanyua mashabiki wa Yanga dakika ya 64.
Dakika ya 40 kipindi cha kwanza Ramadhani Kabwili mlinda mlango wa Yanga alitolewa akiwa kwenye machela baada ya kuumia, nafasi ilichukuliwa na Klaus Kindoki, mchezo wa mwisho kudaka ilikuwa dhidi ya mwadui FC ambapo alitolewa nafasi yake ikachukuliwa na Ramadhan Kabwili.
Jafari Mohamed alitoka pia dakika ya 40 baada ya kuumia akaingia Deus Kaseke kuchukua nafasi.
Hii Yanga ni ya pekee!...wako only 15 ambao wanacheza wengine wengi ni majeruhi na wana matatizo mbalimbali lakini waliobaki wanacheza kwa ujasiri, juhudi maelewano na moyo wa kujituma....na hawana first eleven kila mchezaji aliyesajiliwa anatumika!
ReplyDelete