December 25, 2018


Hii inaweza kuwa haijawahi kutoka katika soka la Tanzania, unaambiwa Yanga imeshatumia takribani jezi nne mpaka sasa katika mechi za ligi.

Hii imetokana na jana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tukuyu Stars ambao ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 kuja na jezi mpya.

Jezi hizo zilemeta mjadala mitandaoni ambapo mashabiki na wapenzi kadhaa wa Yanga wameeleza kuwa Yanga inazidi kujipa hali ngumu yenyewe.

Baadhi wamesema kuwa klabu kwa sasa inapitia wakati mgumu kiuchumi lakini jezi zimekuwa zikitambulishwa kila siku mpya na haijulikani mpaka sasa jezi yake rasmi ni ipi.

Hivi karibuni Kaimu Katibu wa klabu, Omar Kaya, alisema wanaamua wenyewe kuhusiana na suala la jezi zipi watumie na hawewezi kushinikizwa na mtu mwingine yoyote.

4 COMMENTS:

  1. Usiwe na wasi, watabadili wawezavyo but c kwa kuvaa njee ya rangi mama.

    ReplyDelete
  2. mnawasifia kubadili jezi wakati wachezaji wanalia njaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. We unafikiri watawezaje kucheza soka wakiwa na njaa?? Unafikiri kututumuka pale uwanjani ndani ya dk 90 na kupata ushindi watu hawali? Kwa taarifa yako Yanga hata kama imekosa hela kusajili dirisha dogo lakini mdogo mdogo inasonga mbele na ndo maana kauli mbiu "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO". Hela ya kula ipo kaka jezi zipo kibao na bado za kijani zake zimetulia we tupotezee kimtindo kwanza tule Xmas yetu bila kupoteza mchezo...

      Delete
  3. Yanga kuweni wepesi hata kuiga watani zenu
    ....mfano mwezi february ni kumbukumbu ya kuzaliwa klabu ya yanga iteni mechi ya kimataifa ya kirafiki na chezeni mechi ya kimataifa na klabu kongwe moja ya Afrika au Ulaya katika uwanja wa Taifa mjaze uwanja siku hiyo fanyeni umahasishaji nchi nzima na matendo ya fadhila katika jamii waalikeni mabalozi waasisi wa uhuru wa Tanganyika walio hai na wa mapinduzi ya Zanzibar ipigwe dua jangwani....halafu wachezaji watembelee hospitali na kutoa misaada, na pia uwanja wa Taifa kuwe na burudani mbalimbali halafu jioni muujaze uwanja....mtapata fedha nyingi tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic