December 28, 2018


Straika hatari katika kikosi cha Simba, Meddie Kagere, amesema lengo lake ni kufunga mabao zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika 'CAF Champions League.

Kagere ambaye tayari ameshacheza na nyavu mara tatu, ameeleza pale atakapokuwa anapata nafasi basi ni lazima azitumie vema.

Mchezaji huyo amefunguka kuendelea kupambana kadri awezavyo ili aache historia kwenye mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu Afrika.

"Lengo langu ni kufunga mabao, nitafanya hivyo kila ninapopata nafasi" alisema.

Mrwanda huyo katika Ligi Kuu Bara msimu huu tayari ameshaweka kambani jumla ya mabao 7 na akiwa kwenye kikosi cha kwanza cha wekundu wa msimbazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic