December 28, 2018


Mshambujiaji wa Yanga, Amissi Tambwe, amedhamiria kuibeba timu yake hiyo msimu huu baada ya kusema atahakikisha msimu ujao inashiriki michuano ya kimataifa kama zamani.

Tambwe raia wa Burundi, ametoa kauli hiyo baada ya kuiwezesha Yanga kufuzu Hatua ya Nne ya Kombe la FA baada ya Jumatatu iliyopita kufunga
mabao matatu katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Tukuyu Stars, huku timu hiyo ikiwa inaongoza Ligi Kuu Bara na pointi zake 47.

Kwa misimu ya hivi karibuni, Yanga imekuwa ikishiriki michuano ya kimataifa mfululizo lakini msimu huu imeikosa nafasi hiyo kutokana na kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

“Msimu ujao tunataka kushiriki michuano ya kimataifa, hivyo nitaipambania timu yangu mpaka tufi kie malengo hayo. Hatutaki kurudia makosa kama yale ya msimu uliopita.

“Hivi sasa tumefuzu hatua inayofuata katika Kombe la FA, moto ambao tumeuonyesha tunataka kwenda nao mpaka tuwe mabingwa,” alisema Tambwe. Inafahamika kuwa, bingwa wa Ligi Kuu Bara anashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na bingwa wa Kombe la FA, anashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic