December 20, 2018


Mshambuliaji tegemeo wa Yanga Mkongomani, Heritier Makambo ameshindwa kujizuia na kumwagia sifa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu ambaye amemtaja amehusika mara nyingi kwenye mabao yake msimu huu.

Hadi sasa Makambo amefunga mabao 9 akichuana vikali na mshambuliaji wa Mbeya City, Eliud Ambokile na Said Dilunga wa Ruvu Shooting wote wenye idadi sawa ya mabao.

Wakati, Makambo akifunga idadi hiyo ya mabao, Ajibu yeye tayari hivi sasa amepiga ‘assisti’ 11 ni mchezaji anayeongoza kwenye upigaji pasi hizo za mwisho katika msimu huu wa ligi.

Kwa mujibu wa Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Makambo alisema anafurahia upigaji wake mzuri wa krosi na mipira mizuri ya faulo ambayo imekuwa ikimrahisishia yeye kufunga mabao kama alivyopiga mchezo na Ruvu Shooting.

“Nimpongeze Ajibu kwa uwezo wake mkubwa wa kutengeneza mabao kutokana na krosi na pasi nzuri ambazo amekuwa akizitengeza kwa wachezaji wote.

“Mfano mchezo wetu uliopita wa ligi tulipocheza Ruvu, nilikata tamaa ya kufunga bao kutokana na ugumu wa mechi hiyo, lakini nikafunga bao na hizo zimetokana na juhudi za Ajibu,” alisema Makambo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic