Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na kampuni yakubashiri michezo nchini ya SportPesa leo wamekabidhi zawadi ya Bajaj kwa mshindi wa 84 ya promosheni ya SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA ambayo imekuwa ikiendelea tangu Septemba mwaka huu.
Promosheni ya SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA ni promosheni kwa ajili ya wateja wa SportPesa na Airtel ambapo mshindi anaweza kujishindia TVS KING mpya, pesa taslimu au vyote kwa pamoja.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi Bajaj hiyo kwa mshindi huo wa 84 ambaye ni Abdul Ahmed mkazi wa Mikocheni jijini Dar es Salaam na mfanyabiashara, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema kuwa mpaka sasa SportPesa imeweza kubadilisha maisha kwa Watanzania zaidi ya 90 kwa kujiongezea kipato cha kila siku kupitia bajaj ambazo wengi wao wameweza kuzitumia kwa ajili ya biashara.
Nia yetu sisi SportPesa ni kuendelea kuinua na kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia michezo, alisema Tarimba.
Huyu hapa leo ni mshindi wetu wa 84, mpaka mwisho wa promosheni yetu tutakuwa tumetoa jumla ya Bajaj 100. Kila siku kuna Mtanzania anabadilisha maisha kwa kujishindia Bajaj.
Hii ni mara ya pili kwa kampuni hiyo kuendesha promosheni kama kwa wateja wake. ‘Mwaka jana tuliendesha promosheni kama hii – Shinda na SportPesa ambapo tulitoa bajaj 100 kwa washindi wetu. Washindi walitoka kwenye mikoa yote 23 ya Tanzania na waliweza kubadilisha maisha.
Kwa kupitia Shinda Zaidi na SportPesa, tutaendelea kubadilisha maisha ya Watanzania kwa kupitia kushinda Bajaj pamoja na zawadi zingine. Ninayo furaha kuwa SportPesa imekuwa ikibadilisha maisha ya Watanzania kiuchumi kwa kupitia michezo, alisema Tarimba huku akiongeza kuwa ili kushiriki kwenye promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa na kushinda Bajaj mpya au pesa taslimu, mteja atatakiwa kubashiri kwa kuanzia TZS1000.
“Kama bado hujawahi kucheza na SportPesa basi hakikisha unajisajili kwa kupiga *150* 87# baada ya hapo utatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa kwa namba ya biashara 150888 kisha piga *150*87# au tembelea www.sportpesa.co.tz KUWEKA UBASHIRI wako mara nyingi zaidi ili uweze kuingia kwenye droo, alisema Tarimba.
Kwa wake, Meneja Biashara wa Airtel Money Fidelis Kaijage alitoa wito kwa wateja wa Airtel kubashiri kwa kutumia Airtel Money ili kujihakikishia ushindi mara mbili, bajaj pamoja na fedha taslimu.
Kwa kubashiri kutumia Airtel Money, mteja atakuwa na uwezo wa kushinda mara mbili. Kile ambacho mteja anachotakiwa kufanya ni kujiandikisha, kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kwa kutumia Airtel Money halafu ndio abeti, alisema Kaijage.
0 COMMENTS:
Post a Comment