Mkwasa ambaye hivi sasa anaendelea vizuri na hali yake kiafya baada ya kufanyiwa vipimo huko India miezi kadhaa iliyopita, ameeleza Simba wanapaswa kujiandaa kisawasawa.
Katibu huyo wa zamani Yanga, amewaasa Simba kujipanga vilivyo ili waje kufanya vizuri kwa kuonesha jitihada zenye malengo changa ili waweze kushinda.
Aidha, Mkwasa amesema mechi za makundi zote ni ngumu kulingana na timu zote zilizofikia katika hatua hiyo kuwa ni bora.
"Hakuna mechi rahisi, Simba wanapaswa kujipanga vilivyo na wafanye mazoezi ya maana waje kufanya vizuri kwa kuiwakilisha Tanzania vema.
"Hakuna mechi rahisi katika makundi yote, kwani ubora wa timu zote zilizofika kwenye hatua hiyo unajulikana", amesema Mkwasa.








0 COMMENTS:
Post a Comment