MCHEZAJI SIMBA ATOA ONYO KWA WACHEZAJI KUHUSU CAF
Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na klabu ya Simba, Madaraka Selemani, amewataka Simba kujiandaa kisaikolojia kwa kutumia vema uwanja wa nyumbani kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Seleman amewataka Simba kufanya hivyo ili wanufaike kama ambavyo walifanikiwa kwa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa kuichakaza kwa jumla ya magolo 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkongwe huyo ambaye alitamba kwenye soka la miaka hiyo ana imani Simba wakipamba vema Dar es Salaam basi katika michezo ya marudiano kama wataanzia nyumbani hawatapa tabu.
"Simba wanapaswa kujipanga vema na haswa wajitahidi kutumia zaidi faida ya uwanja wa nyumbani kwani itawasaidia kupenya kirahisi kwa mechi ambazo wataanzia Dar es Salaam" alisema Seleman.
Katika kundi D Simba ipo na moja ya klabu ambazo ni Al Ahly ya Misri na AS Vital ya Congo ambazo zote ni moto wa kuotea mbali.








Kwanini Tanzania tumepoteza wachezaji kaliba ya akina Madaraka Suleiman? Nini kimetufika? Ukizungumzia watu wagumu,wanaume wagumu,fowadi ngumu wenye kulazimasha mabao beki itake isitake basi Madaraka Suleiman ni aina ya wachezaji waliotoweka kabisa katika soka la Tanzania. Sasa hivi unaweza kusema Meddy Kagere ni miongoni mwa fowadi wagumu lakini mbele ya Madaraka Suleiman enzi zake,Kagere ni cha mtoto sana. Kundi la Simba watu wengi wanalichukulia poa lakini kiukweli ni kundi hatari sana ni kundi la kifo hasa na si ajabu bingwa akatokea kwenye kundi hili. Wale Wa Algeria ni full of surprises kama walivyo Simba ni Underdogs lakini wamezamiria kufanya kufuru kwenye hatua hii ya makundi na kufika mbali. Al Ahly ya Misri baada ya kupoteza mwchi ya ubingwa mbele ya Esperence ya (Tunisia) ni kama vile mtu aliekwenda safari akapotea na kuja kufahamu kilichompoteza na kuianza safari hiyo kwa hasira huku akiwa na uhakika na anapotaka kwenda na hakuna kitakachomzuia na anapotaka kufika. As Vita ni ya (Congo DRC) ni vita Kweli sio mchezo ikichagizwa na hamasa ya hali ya juu baada ya kubeba kombe la shirikisho hivi karibuni. Ni moja ya timu hatari sana kwa Simba kwa sababu wana urahisi wa kupata taarifa nyingi za Simba kwa wepesi zaidi kuliko wapinzani wake wengine katika kundi hilo. Licha yakuwa timu ya nchi jirani lakini wana mtu kama Mwinyi Zahera kocha wa Yanga na kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo ambao ndani ya As Vita kuna wachezaji wake wa timu ya Taifa pia. Kwa hivyo Simba lazima wajiandae kupitia kunako tanuri la moto kabla ya kutamani ushindi kutoka kwa wapinzani wake hao la sivyo itakweta kuwathibitishia watu kuwa Simba ni wanyonge katika timu nyonge katika mashindano hayo na kwa kuwa inatokea Tanzania. Ninachokiamini mimi huu ni wakati wa kujiapiza watanzania sio Simba tu bali watanzania na Tanzania kwa ujumla kama alivyojiapiza kiongozi wetu as nchi muheshimiwa Raisi Maghufuli kuwa unyonge basi tena watanzania tunaweza. Na ni vizuri kwa Simba kabla ya kuanza hatua ya makundi ni vyema kwenda kuonana na Muheshimiwa rais Magufuli na hakuna siasa katika hili bali Simba wakati huu wanahitaji sana kiwango kikubwa cha (Inspiration) au hamasa ili kuwajenga kisaikolojia yakuwa wanaweza bila ya shaka yeyote na kama kuna mtu au kiongozi asie na hofu na wala shaka na kile anachotaka kukikamilisha kwa sasa basi hakuna kama Magufuli katika Taifa hili pengine Africa na Duniani kwa ujumla ni bahati kuwa na kiongozi tulienae hivyo lazima tumtumie pia kukamilisha malengo yetu na tusiishie kumsifia tu na nadhani hata hii morali ya sasa ya Simba kwenye mashindano haya ni wazo lake. Sasa nadhani ingelikuwa busara kwa Simba kwenda kuonana nae na kupata mawazo mapya yatakayokoleza hamasa ya kupambana ili kupata ushindi na kama Mzee mwenyewe atawakubalia kuonana nao na kama atakuwa na nafasi kwa sababu tayari alishavunjwa moyo na Taifa Stars. Ila nnaimani Mzee mwenyewe atakuwa anaifuatilia Simba kwa karibu kwenye mashindano haya kuona maagizo yake yametiliwa uzito kwa kiasi gani na so far nadhani Simba wanaendana na maagizo yake ila kazi ndio Kwanza imeanza kwa hivyo kujipanga vilivyo ni lazima. Kuhusiana na faida ya uwanja wa nyumbni lazima Simba waandae mazingira ya uwanja wa Nyumbani kuwa kaa la moto kwa timu pinzani na wasisubiri michuano hiyo kuanza bali waanze kuwahamasisha mashabiki wake kuanza hamasa hizo kwenye michezo yao ligi kuu. Mazembe moja ya kitu kinachowabeba ni wingi wa hamasa za Mashabiki wake, Al Ahly vile vile nakadhalika nakadhalika. Heri ya mwaka mpya
ReplyDeleteKama Simba itaenda makundi kwa kumtegemea Boko,Gyan na Shabalala itakuwa imechezea nafasi. Ktk mipira 20 Boko anafunga 1.
ReplyDeleteBora mara mia tukamuazima Tambwe maana anajua kucheza na nyavu na akipata assistance ya Chama basi ktk magoli matatu ya wazi ni lazima atatupia moja.
DeleteNi kweli bokko bado kabisa na beki ya gyan na shabalala ni wabovu Jana nimeona ni uchochoro kabisa.tunahitaji straker wa mana na mabeki 2.
ReplyDeleteBeki mmoja wa kati anahitajika awe na misuli kama mnyarwanda Abdul au Yondan.Beki ya kushoto Tshabalala hana nguvu na ukikumbuka Nkana walikuwa wanacheza sana upande wa Tshabalala baada ya kuona madhaifu na sielewi kwa nini Asante Kwasi is not a starter kwenye mechi za siku hizi.Gyan kiasilia si beki na hizi timu tutakazocheza ktk kundi D sio la mchezo hata kidogo.Kama kweli timu zinaruhusiwa kuongenza wachezaji 3 basi ni muhimu sana wakaongezwa.
ReplyDeleteKwasi alikuwa Majeruhi kwa majuma kadhaa kwa hiyo hajawa fiti 100%
ReplyDelete