RUVU SHOOTING WAJIANDAA KUIFANYIA UMAFIA HUU SIMBA KWENYE LIGI
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameibuka kivingine kwa kusema kuwa malengo yao hivi sasa ni kuwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kauli ya Masau imekuja kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United jana kwenye Uwanja wa Mlandizi huko Pwani.
Masau anaamini kwa namna kikosi chake kilivyo hivi sasa wana ndoto za kuwa mabingwa kwa kupambana kufa na kupona ili watimize lengo hilo.
Ruvu baada ya ushindi wa jana imefikisha jumla ya alama 20 kwenye msimamo wa ligi huku Yanga iliyo kileleni ikiwa na 50 pamoja na Azam iliyo nafasi ya pili ikiwa na 40.
Vilevile Simba ambao ni mabingwa watetezi wako kwenye nafasi ya 3 wakiwa na pointi 33 wakicheza michezo 14 pekee.
"Tumejipanga vilivyo, tutapigana ikiwezekana tuweze kuchukua ubingwa wa ligi kuu kwa msimu huu, naimani inawezekana" alisema Masau.
Masau Bwire haishigi karana za maneno ila atakapokutana na Simba basi asije kukimbilia kukipapasa cha moto chake mpira ni utani bhana hata ukifungwa vumilia.
ReplyDeleteHivi kamati ya nidhamu mbona haitoi taarifa dhidi ya wacjezaji waliopelekwa huko. Au inasubiri ligi iishe
ReplyDelete