December 31, 2018


Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems, amesema mchezaji wake mpya kutoka Burkina Faso, Zana Coulibaly anahitaji muda kuzoea kikosi chake.

Aussems ameamua kufunguka baada ya mashabiki wa timu kuanza kumtupia lawama wakati akiwa ana muda mfupi pekee.

Beki huyo aliyekuja Simba kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Shomari Kapombe, ameanza kurushiwa maneno na baadhi ya mashabiki kuwa hana uwezo mzuri uwanjani.

Licha ya lawama hizo, Mbelgiji Aussems amepingana nao na kusema kuwa anahitaji muda kwani ana uwezo na uzoefu wa soka la kimataifa.

Coulibaly mpaka sasa amechacheza jumla ya mechi tatu tangu atue Msimbazi ikiwemo mbili za Ligi Kuu Bara na moja ya Kombe la FA.

3 COMMENTS:

  1. Coulibaly ni beki mzuri sana tu ningewashauri mashabiki wa Simba wasiwe wavivu na wajaribu kuyutube na kumuangalia zana coibaly akicheza mechi za ushindani kabla ya kuja Simba. Mashabiki wanatakiwa kuwa wavumilivu na sio kumnyoshea kidole cha lawama mchezaji badala yake wanatakiwa kuwasapoti.

    ReplyDelete
    Replies
    1. anaonekana ni mzito kumaanisha huenda aikaa benchi kwa muda lakni ukimuangalia anaonekana kweli anajiamni kumaanisha ni mchezaji mzeofu dimbani

      Delete
  2. Ni mchezaji mzuri sana na ataisaidia Simba kimataifa. Mara nyingi ubora wa mchezaji huonekana baada ya muda. Kumbuka mchezaji kama Obrey Chirwa alivyoingia Yanga wengi walimponda lakini baada ya muda aliwa-prove wrong waliokuwa wanamkosoa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic