Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar, ambayo inashiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika umesema kuwa utamtumia aliyekuwa Kocha Mkuu wa zamani wa timu ya Taifa, Salum Mayanga ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa benchi la ufundi katika timu hiyo.
Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuona wanapata matokeo katika mchezo wao dhidi ya KCCA ya Uganda kati ya Desemba 14 au 15.
"Mipango ipo sawa na benchi la ufundi linafanya jitihada kuwaweka vijana sawa, tunamtumia Mayanga katika kuwapika vijana kwa kuwa anauzoefu na michezo mingi ya kimataifa akisaidiana na Kocha Mkuu, Zuber Katwila," alisema.
Mtibwa wamefanikiwa kupenya hatua ya awali baada ya kuifunga Northen Dynamo ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 5-0, mechi ya kwanza hatua ya kwanza wataanzia ugenini.
0 COMMENTS:
Post a Comment