Mbabe wa washambuliaji wa kigeni kwenye ligi Kuu Tanzania Bara, Eliud Ambokile ambaye ni mzawa amesema kuwa kikubwa kinachomfanya aweze kufanya vizuri ni kujiamini akiwa uwanjani na kutokata tamaa kutafuta nafasi.
Ambokile anayeitumikia Mbeya City kwa sasa ni kinara wa mabao akiwa amefunga mabao 9 na timu yake ikiwa imecheza michezo 15 mpaka sasa huku mfungaji bora wa msimu uliopita na mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akiwa na mabao 7 huku timu yake ikiwa imecheza michezo 12.
"kila mara nafikiria kuweza kuisaidia timu yangu kupata matokeo hivyo kila nikipata nafasi nafunga kwa kuwa sikati tamaa nikiwa ndani ya uwanja na ushirikiano uliopo unatujenga zaidi," alisema.
Washambuliaji wengine ambao wana mabao mengi ni pamoja na Saidi Dilunga wa Ruvu Shooting mabao 8 sawa na Herieter Makambo wa Yanga huku Okwi na Kagere wa Simba wana mabao 7.
0 COMMENTS:
Post a Comment