December 28, 2018


Ligi Kuu Tanzania Bara imeendelea leo huku timu nane zikitimiza majukumu yao kutafuta pointi tatu, timu moja tu imefanikiwa kubeba pointi tatu huku nyingine zikigawana pointi moja moja kwenye viwanja tofauti.

Tanzania Prisons ya Mbeya imetoka sare ya bila kufungana na Coastal Union ya Tanga uwanja wa Sokoine Mbeya na kufanya wagawane pointi 1.

Kagera Sugar imeibuka kidedea dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa uwanja wa Kaitaba, bao lilifungwa dakika ya 45 na Omary Daga.

Stand United wamekubali sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Alliance ya Mwanza wakiwa nyumbani katika mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga, Alliance walifunga bao dakika ya 24 kupitia kwa Dickson Ambuda na lile la Stand United kupitia kwa Hafidhi Mussa dakika ya 90.

KMC wanakubali sare ya kufungana dhidi ya Mbao FC katika mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru, KMC walianza kuandika bao dakika ya 45 kupitia kwa Emmanuel Mveyekule na Mbao walisawazisha kupitia kwa David Mwassa dakika ya 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic