December 13, 2018

Mwakilishi wa La Liga nchini, Luis Cardenas leo Alhamisi, Desemba 12, 2018 ametembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayofanyika katika ofisi hizo. Ofisi za Global Group zinajumuisha kampuni ya mbalimbali zikiwemo Global Digital na Global Publishers inayochapisha magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra. Luis Cardenas amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata na kuahidi kuendelea kushirikiana na Global Group katika masuala mbalimbali.


Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kushoto) akizungumza jambo na Luis Cardenas. Luis Cardenas akisoma Gazeti la Spoti Xtra lililotoka leo Alhamisi.
  Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph akisalimiana na Luis Cardenas. Akisalimiana na Mhariri Msadizi wa Championi Jumamosi, Omary Mdose. Mhariri wa Championi Jumamosi, Lucy Mgina akisalimina na Luis. ...Saleh Ally (kushoto), Luis na Lucy Mgina wakisoma Gazeti la Championi. Luis akiongea na Mwandishi wa Gazeti la Championi na Spoti Xtra, Wilbert Molandi (kushoto) wakisikilizwa na Saleh Ally (kulia). Saleh Ally akimuonyesha Luis jinsi Gazeti linavyoandaliwa
  Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, Luis Cardenas leo Alhamisi alipotembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic