December 13, 2018



Tayari Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amepitisha uamuzi kwamba kiungo mshambuliaji Ruben Bomba asisajiliwe.

BONYEZA HAPA KUJIUNGA NASI INSTAGRAM ==> SALEH JEMBE SPORTS
Bomba alikuwa anasubiri kusajiliwa na Yanga baada ya mwenyewe kumleta. Lakini sababu kuu mbili zimemfanya apitishe uamuzi huo.

MOJA:
Zahera ameona, Bomba hana kile kiwango alichokuwa anakijua. Maana yake analazimika kutengenezwa. Pia, Bomba alikuwa hataki kuanza mazoezi hadi atakaposajiliwa na alipolazimishwa kuanza, Zahare akashituka.

PILI:
Zahera alishauri Bomba kusajiliwa kwa fedha ya bei nafuu, ili amrudishe katika kiwango chake.

Kwa kiungo huyo ameona ni ndogo kama amedharauliwa. Akasema yeye ni mchezaji mkubwa na kiwango kilichopendekezwa ni kama kumdharau.

Unaambiwa, Zahera akasema basi poa, mlango mweupe anaweza kurejea DR Congo nyumbani, “watakutanaga”.

Njoo vile.
 

BONYEZA HAPA KUJIUNGA NASI INSTAGRAM ==> SALEH JEMBE SPORTS

3 COMMENTS:

  1. Hivi kweli hajala pesa yetu ya kukaa gesti? Yanga tunahujumiwa ila tutavuka.

    ReplyDelete
  2. Duuu! Hivi hii Yanga yenu haina Ma-Economist? Lakini haya ndo mwendo huo. Msiamini kila litokalo kinywani mwa mwaminifu.

    ReplyDelete
  3. Kwanini huyu Kocha analeta wachezaji au wachezaji wanapendekezwa na kutumiwa nauli na kukaa hotelini halafu hawasajiliwi...hapa kuna either shida ya scouting makubaliano ya fedha au usanii...lazima katika hili Takukuru iingilie na idara ya uhamiaji hapa kuna kitu inawezekana hawa wanakuja kutalii tu..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic