Imeripotiwa kuwa Mahakama Kuu jijini Dar kitengo cha Biashara imemuamuru Mfanyabiashara Yusuf Manji na Wenzake kulipa kiasi cha fedha Bilioni 33 kwa benki ya NBC kutokana na mkopo waliochukua katika matukio tofauti
Katika kesi namba 54 ya 2018, Manji na Washtakiwa wengine, Farm Equip(Tanzania) Company Limited, Tanperch Limited, Quality Group Limited na Kaniz Manji wanatakiwa kulipa jumla ya Tsh. 15,982,193,605.23
Kwenye kesi namba 56 ya mwaka 2018 ambapo Washtakiwa ni Manji, Tanperch Limited, Quality Group Limited na Kaniz Manji, wanatakiwa kuilipe NBC jumla ya USD 5,468,274.23 kama riba ya marejesho ya Mkopo
Aidha, katika kesi nyingine namba 55 ambapo Washtakiwa ni Quality Corporation Limited, Quality Group Limited, Tenperch Limited, Yusuf Manji and Kaniz Manji, Mahakama imeamuru walipe Tsh. 5,359,418,687.31.
Hii ni habari ya michezo kweli ndugu
ReplyDeleteSi mwanamichezo huyo au unajitoa fahamu
DeleteHabari Haieleweki Kichwa Wala Miguu
ReplyDeleteUsijifanye kizibo,nin kisichoeleweka hapo?wewe tambua manji anadaiwa basi,manji ni mdau wa soka
ReplyDelete