Kocha Masoud Djuma anaamini kikosi chake cha AS Kigali kitang'oka katika nafasi ya mkiani katika Ligi Kuu Rwanda.
AS Kigali inayofundishwa na kocha huyo wa zamani wa Simba, inashika nafasi ya 14 katika timu 16.
Djuma aliyewahi kuinoa Simba kama kocha msaidizi na kocha mkuu kwa muda, amesisitiza kwamba anaendelea kupambana.
"Kweli hali si nzuri lakini naendelea kupambana ndugu yangu. Unapokuwa unapitia mengi ndio kujifunza na kukua kwenyewe," alisema.
AS Kigali ni moja ya timu kongwe za Rwanda lakini kubwa na tajiri kama ilivyo kwa APR na Rayon Sports yenye mashabiki wengi zaidi nchini humo.
Kabla Djuma, aliwahi kuichezea APR lakini aliwahi kuwa kocha aliyepata mafanikio makubwa akiinoa Rayon Sports.
huyu si ndio alitaka apewe ukocha mkuu wakati Simba inaendelea kupasua anga yeye anapigania kuepuka kushuka daraja
ReplyDelete