Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire, jana aliamua kutoa bastola uwanjani ili kuwazuia mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakimzonga na kumkejeli.
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, ulisababisha mashabiki wengi wa Yanga kuanza kumtania Bwire ambaye alikuwa ameyapokea matokeo kwa masikitiko.
Bwire amefunguka kuwa aliamua kufanya maamuzi hayo ili kuwatawanyisha mashabiki hao na kweli alifanikisha azimio lake baada ya kukimbia haraka.
Baada ya matokeo hayo, Yanga ilizidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha jumla ya alama 44 huku wa pili Azam akiwa na 40.
0 COMMENTS:
Post a Comment