December 17, 2018


Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imetoa ushauri kwa klabu za Simba na Mtibwa kujipanga vema kuelekea mechi za marejeano za mashindano ya kimataifa.

Kupitia Waziri mwenye dhamani, Harisson George Mwakyembe, amesema kupoteza katika mechi za kwanza ambazo walicheza ugenini isiwe sababu ya kukata tamaa mapema.

Mwakyembe amewamua kuwapa nguvu Simba na Mtibwa ili waweze kujipanga vizuri kuelekea mechi za marejeano akiamini lolote linaweza kutokea ndani ya dakika 90.

"Nawasihi vijana wetu wapambane na wajipange kuelekea mechi za marudiano, sikutegemea kama wangeweza kupoteza kulingana na namna walivyofanya vizuri katika mechi za kwanza" alisema.

Katika mchezo ambao Simba walicheza dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia walipoteza kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Mtibwa akipoteza kwa mabao 3-0 kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba itarejeana na Nkana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Disemba 23 sambamba na Mtibwa ambayo watacheza na KCCA pale Azam Complex tarehe sawa na mechi ya Simba.


1 COMMENTS:

  1. Upande Wa Mtibwa Sina Hakika Kama Wananafasi Ya Kubadili Chochote Labda ! Tusubiri. Angalau Simba Wananafasi Ya Kushinda Maana Wao Wana Hitaji Goal 1 Kwa 0 Tu, Tofauti Na Wenzetu Mtibwa Sugar Wanao Hitaji Goal 4 - 0 Si Mchezo Na Kibaya Ni Kwamba Wachezaji Wao Sidhani Kama Wanauwezo Binafsi Kwa Kuipa Mtibwa Matokeo Ya Ajabu Ya Kupindua Meza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic