Kocha wa timu ya Lipuli ya Iringa Seleman Matola amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kimeanza kuimarika hivyo ana uhakika wa kupata matokeo katika michezo yake inayofuata ya Ligi Kuu.
Matola jana alifanikiwa kuipapasa Ruvu Shooting katika uwanja wa nyumbani wa Samora kwa ushindi wa mabao 2-1.
"Ni mipango na juhudi za vijana wakiwa uwanjani, kila siku kuna mabadiliko na ushindani uliopo unawafanya wajitume imani yangu watafanya vizuri michezo yao ijayo," alisema.
Mabao ya Lipuli yalifungwa na Miraji Adam huku lile la Ruvu Shooting likifungwa na Said Dilunga na kuifanya Lipuli kupanda kutoka nafasi ya 15 mpaka ya 10 baada ya kufikisha pointi 19.
0 COMMENTS:
Post a Comment