Kocha mkuu wa KMC, Ettiene Ndayiragije amesema kwamba kikubwa kinachoikwamisha timu yake kushindwa kulinda matokeo yake ni wachezaji kukosa uzoefu baada ya kutangulia kufunga dakika ya 18 kupitia kwa George Sangija na dakika ya 63 kupitia kwa Rayman Mgungila.
KMC walikuwa wakiongoza dhidi ya Azam FC katika mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 ambapo bao la Azam FC la kusawazisha la kwanza lilifungwa dakika ya 45 na Tafadzwa Kutinyu na lile la pili lilifungwa na Donald Ngoma dakika ya 85.
Ndayiragije amesema wachezaji wake wanazidi kuimarika taratibu ana imani watampa matokeo mazuri wakati ujao kwa kurekibisha makosa wanayoyafanya kwa sasa.
"Bado kuna tatizo kwa wachezaji wangu kukosa uzoefu wa kuweza kushambulia pamoja na kulinda ushindi, mpira una kanuni haina maana ukitangulia kushinda wewe ndiye mshindi unapaswa usubiri dakika 90 zimalizike," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment