Baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Azam
FC kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0 uongozi wa timu ya Mbao umebainisha
kilichowaponza kupokea kichapo ni kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.
Mbao walifungwa na Azam FC katika uwanja wa
Chamazi uliochezwa majira ya saa moja usiku na kuwafanya Azam FC waweze
kujikita kileleni baada ya kufikisha pointi 39 wakiwaacha Yanga kwa pointi 1.
Mwenyekiti wa
Mbao, Solly Njash amesema matokeo waliyopata yamewaumiza kwa walijipanga sawasawa kupata matokeo, wamerejea Mwanza kujipanga upya.
"Tumepoteza mchezo wetu dhidi Azam FC,
hatupo sawa na tunajua mashabiki wetu wameumia kwa matokeo hayo hatuwezi kumshushia mtu lawama kwa kuwa ni matokeo.
"Tulipata nafasi kwenye mchezo na
tukashindwa kuzitumia hivyo nafasi zitabaki kwenye mdomo ila matokeo ndio
yameshatokea hakuna namna nyingine," alisema.
Mbao inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 15 ikiwa imejikusanyia pointi 20 imekubali kupoteza mchezo huo ambao ulikuwa ni kiporo.
0 COMMENTS:
Post a Comment