December 15, 2018


Na George Mganga

Meneja wa kipa namba moja wa Yanga, Beno Kakolanya, Seleman Haroub, amesema kazi ya uwakala inahitaji ueledi na si ushabiki kama baadhi wanavyodania.

Kwa mujibu wa Radio One, Seleman amesema hayo kutokana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, hivi karibuni kuibuka akielezwa kushangazwa na kipa wako Kakolanya kuwa na wakala ambaye anafanya kazi katika klabu ya Simba.

Zahera alieleza kuwa inashangaza kuona mchezaji wa Yanga anaongozwa na wakala ambaye anafanya kazi Simba huku akiamini ndiyo sababu iliyopelekea Kakolanya akakacha mazoezi Yanga.

Seleman amejibu kauli za Zahera akisema kazi ya uwakala inachukua sehemu yake na kama yeye yupo Simba si sababu ya kushindwa kumsimamia Kakolanya.

"Unajua suala la uwakala linakuwa sehemu yake, mimi kufanya kazi Simba haiwezi pelekea nikawa msimamizi wa mchezaji kutoka timu nyingine, si mambo ya ushabiki haya, kikubwa ni kuonesha ueledi wa kazi" alisema.


5 COMMENTS:

  1. Si kwa sis Watanzania...tunapenda timu zetu kuliko maelezo

    ReplyDelete
  2. Ikitokea simba na yanga wanataka kumsajili beno kukawa na ushindani mkubwa hutompeleka simba? Wakala anatakiwa kutokuwa kiongozi wa club anaweza kuwa shabiki tu

    ReplyDelete
  3. Tuache ushabiki maandazi nani anamjua wakala wa emmenuel okwi ni kiongozi wa sport club villa na mara nyingi amekuwa akiwa villa okwi akipata timu nyingine huwa anaoondoka tu bila shida yeyote mpira kwa mchezaji ni kazi sio ushabiki ata wakala kwake ni kuangalia masilahi sio ushabiki tuache mambo ya kishabiki kocha wa yanga nae kaingia kwenye mkumbo wa ushabiki sio weledi sasa yeye anahisi beno atakosa timu

    ReplyDelete
  4. Leo beno anaonekana msaliti na analeta usimba kisa kudai haki yake,vipi kuhusu yondani amegoma Mara ngapi,amerud kambin mbona zahera hajamfukuza,aache ushamba was kumhis MTU vibaya,angekuwa simba ile mechi na simba yet ndio walmwimba kuwa shujaa,leo anadai haki yake kawa zero,kawa simba,pu.....mbavu

    ReplyDelete
  5. Unknown mbona unaongea peke yako unauliza na kujijibu mwenyewe? kama humjui Wakala wa Okwi sema tukusaidie tunaeishi naye sio kutoa hoja usizozijua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic