December 24, 2018


Baada ya kuondoshwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Mtibwa Sugar ya Morogoro imeweka wazi kwamba hasira na nguvu zao wanaziweka kwenye ligi kuu ambapo wataanza kwenye mechi yao ya wiki hii dhidi ya Azam FC.

Mtibwa walitupwa nje ya Kombe la Shirikisho na Waganda KCCA kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya kufungwa kwenye mechi zote za nyumbani na ugenini.

Kocha wa Mtibwa, Zubeir Katwila amesema kwamba sasa macho yao yote wanaangalia kwenye mechi zao za ligi kuu ili kupata ushindi ikiwa ni baadaya kujifunza mambo mengi kwenye kombe hilo waliloshiriki.

“Sasa tunageukia ligi kuu na lengo ni kufanya vizuri katika kila mechi ikiwa ni baada ya kupata mambo mengi kwenye Kombe la Shirikisho ambapo tumeshiriki.

“Tunatambua kwamba ugumu ambao tutakutana nao kwenye mechi hiyo lakini kwa sababu tunataka kushinda tutajitahidi kupambana ili tutimize kile ambacho tunakitaka,” alisema.

Mtibwa wataikaribisha Azam FC inayofundishwa na Mholanzi Hans van Der Pluijm katika mechi itakayopigwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic