December 24, 2018



Kocha wa Lipuli, Seleman Matola ameshangazwa na uwezo wa Simba kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka 2003 kipindi akiwa ni mchezaji wa timu hiyo na amewapa kazi ngumu ya kufanya kimataifa.

Matola amesema Simba imewashangaza wengi kwa kupindua meza kibabe hali iliyowatoa kimasomaso mashabiki wa Simba na Taifa kiujumla.

"Ni jambo kubwa ambalo wamelifanya na wanastahili pongezi kwa kuwa wamevunja rekodi ambayo iliwekwa, sasa wana kazi mpya ya kuweka rekodi nyingine katika mashindano ya kimataifa.

"Rekodi zimewekwa ili zivunjwe kwa hali ambayo ipo sasa Simba wana mtihani mzito wa kusonga mbele kimataifa ili wafanikiwe wanapaswa kuongeza zaidi juhudi na kuacha kiburi cha mafanikio ya muda," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic