MWANACHAMA YANGA ALIYETANGAZWA KUFUATILIWA NA DOLA KISA UCHAGUZI AIJIBU SERIKALI
Mwanachama wa Yanga aliyetajwa katika orodha ya majina ambayo yanapaswa kuchunguzwa na dola, Kais Edwin, ameibuka na kujitetea akieleza lengo lao ilikuwa ni kutaka uchaguzi wa klabu usimamiwe na kamati yao ya uchaguzi.
Edwin ambaye ametajwa katika orodha ya wale ambao wanapinga uchaguzi wa Yanga kufanyika, amesema hawakuwa na nia mbaya na wala si kuwa hawataki kufanyika uchaguzi bali hawakuwa tayari kusimamiwa kupitia Kamati ya TFF.
Mapema jana kupitia Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Yusuph Singo alitangaza kuwachunguza wanachama wanne akiwemo Edwin baada ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuyapata majina hayo usiku wa juzi kuwa wanawashinikiza wanachama wenzao kugomea uchaguzi wa klabu hiyo ambao umepangwa kufanyika Januari 13, mwakani.
"Sisi hatukuwa na nia mbaya bali hatukutaka kuona katiba yetu inavunjwa, hatukuhitaji kamati ya uchaguzi ya TFF isimamie uchaguzi wetu wakati hata sisi tunajitosheleza" alisema.
Maamuzi ya wiazra hiyo yamemuibua Edwin na kueleza kuwa msimamo wao ulikuwa na mashiko na wenye msingi kwakuwa hawakuona ni sahihi katiba ya Yanga kuvunjwa.
Hata hivyo Edwin ameitaka dola ifanye kazi kama serikali kwani hawawezi kupingana nayo na hata kama ikiamua kuwakamata wao wapo tayari.
Wanachama waliotajwa kufuatiliwa na dola ni pamoja na Mustapha Mohammed, Said Bakari, Shaban Omari, Kitwana Kondo Kipwata, Boazi Ikupilika, Bakili Makere, David Sanare na Edwin mwenyewe.
SIMBA WANAJUA KUA HAWAWEZI KUENDELEA KUA MABINGWA WA LIGI BILA KUWATUMIA VIONGOZI WAO WALIOPO TFF NA SERIKALINI KUIANGAMIZA YANGA NA HILO LINAELEWEKA KWA WANA YANGA WOTE
ReplyDeleteKhaa! leo tena Serikali imekuwa ni ya Simba! C ndo nyinyi huwa mnasema Yanga ndio Serikali! imekuwaje tena!Msianze kutafuta visingizio vya kukosa ubingwa mapema hapa. Maana nimeanza kuona visingizio vimeanza kutafutwa na Kocha wenu Zahera, mara ooooh nikiukosa ubingwa msinilaumu kwakuwa uongozi haujasajili kama nilivyoelekeza, wakati yeye ndo alisema kuwa Viongozi wasisajili kwa sababu kuna wachezaji wanaidai timu.
ReplyDeleteSimba hata tukichukua CAF champions league hatutaalikwa bungeni, serikali ni yenu wala msiwe na wasiwasi. Uchaguzi ni lazima timu gani mnataka kuishi bila uongozi? Tff wameingilia kati kwa sababu mmeonesha dhahiri kuwa hsmtaki kufanya uchaguzi.
ReplyDelete