Baada ya mshambuliaji wa timu ya Yanga, Herieter Makambo kuchaguliwa na kamati ya tuzo ya shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuwa mchezaji bora kwa mwezi Novemba, kapteni msaidizi, Juma Abdul ametoa neno kwake.
Makambo amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili ambao ni Said Dilunga wa Ruvu Shooting na Abdallah Shaibu 'Ninja' wa Yanga.
Abdul amesema amestahili kupokea tuzo hiyo kutokana na namna ambavyo amepambana kwa ajili ya kutimiza majukumu yake kwa wakati.
"Ushirikiano ambao tunazidi kuonesha ndani ya kikosi unatufanya tuwe bora, Makambo amefanya kazi ambayo inaonekana na ni jambo la kujivunia hivyo bado ana kazi ya kufanya asiishie hapo.
"Uwepo wake ndani ya kikosi una msaada mkubwa, licha ya kasi yake ya kufunga kuwa ni ya polepole kama wengi wanavyosema, kupewa kwake tuzo kunaongeza morali ya kupambana zaidi," alisema.
Makambo alipata tuzo hiyo baada ya kuweza kufunga mabao 3 katika michezo minne aliyocheza na kuisaidia timu yake kupata pointi 10, na leo watakuwa kibaruani kucheza na Biashara United.
0 COMMENTS:
Post a Comment