Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga imesisitiza suala la Watanzania kuendelea kufaidika kupitia burudani na mengi yanayopatikana katika ligi hiyo.
Mwakilishi wa La Liga aliye hapa nchini, Luis Cardenas amesema kwamba ligi hiyo ni zaidi ya soka pekee.
“Suala la burudani kupitia La Liga ni namba moja lakini La Liga ni zaidi ya mpira pekee kwa kuwa kuna mengi.
“Suala la kuburudika, kuwa pamoja, kujumuika na kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na utamaduni, maisha na kadhalika unaweza kuyapata,” alisema na kuongeza.
“Ukizungumzia suala la ubora kwa takwimu zilizopo sasa, La Liga ndio zaidi duniani. Angalia ubora wa Ulaya na hili halina mjadala.
“Sisi La Liga, tumekuwa tukiendelea kuboresha kila namna ya mambo kama ubora wa viwanja, uhakika wa usalama na kadhalika. Lakini lengo kuu ni kutengeneza kitu kilicho sahihi na kinachowezekana kuwa bora zaidi na zaidi.”
Cardenas amesema Watanzania waendelee kuangalia ligi hiyo bora zaidi ambayo imekuwa ikiendelea kuunda uhusiana na nchi mbalimbali za Afrika na Tanzania sasa ni moja wapo.
Mwakilishi huyo ameendelea kusisitiza kwamba pamoja na Real Madrid na Barcelona, La Liga ina ubora na mvuto kwa kuwa ina timu nyingi kama Atletico Madrid, Sevilla, Valencia na nyingine nyingi zenye ushindani na ubora wa juu.
0 COMMENTS:
Post a Comment