December 28, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuondolewa katika mashindano ya Kombe la FA juzi na Mashujaa United kutoka Kigoma, imebainika Simba hawakuwa na malengo na mashindano hayo ikiwa ni baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-2.

Kupitia Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, jana aliweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo siku za hivi karibuni alionekana akizungumzia malengo ambayo Simba wamejiwekea msimu huu.

Video hiyo ilimuonesha Manara akieleza kuwa Simba ina malengo mawili makubwa pekee msimu ambapo la kwanza ni kuvuka hatua ya makundi barani Afrika katika mashindano a Ligi ya Mabingwa 'CAF Champions League'

Aidha, Manara alisema lengo la pili kwa Simba ni kuhakikisha inachukua ubingwa wa Ligi Kuu huku akijinadi waliokalia usukani wapo pale kwa muda maana watarejea hapo baadaye.

Taswira inaonesha kuwa Simba imeweka nguvu katika mashindano hayo huku hata yale ya SportPesa Super CUP na Mapinduzi inaonekana kama hawatayatilia nguvu.

Kikosi cha Simba hivi sasa kinasubiria droo ya ya kupangwa kwa makundi ya baada ya kuingia hatua hiyo ambapo leo yatafanyika huko Cairo Misri huku Mwenyekiti wake, Sued Kwabi akiwa ameiwakilisha klabu hiyo.

5 COMMENTS:

  1. Simba wameekeza kunako club bingwa Africa hilo halina ubishi na kama wangetolewa na Nkana basi ingekuwa pigo sana hamna maelezo, pengine wangepoteza hata muelekeo wao kwenye ligi kuu. Kitu kimoja nawapa pongezi wanasimba na Simba yao kwa kuwaza makubwa kama vile mtu anaeota kwenda kufunga ndoa akiwa kwenye kinywa cha Mamba mwenye njaa kwa kusema wanataka kuchukua ubingwa wa club bingwa Africa kwani kutokana na ushindani uliopo katika mashindano hayo si mchezo hata kirenki Simba ni miongoni mwa timu kwenye hatua ya makundi yenye rank ndogo na ukiwa na rank ndogo maana yake utapangiwa na alie kuzidi kwa hivyo sio kazi rahisi kuota ubingwa mbele ya Mazembe au Esperence ya Tunisia. Lakini nikimkumbuka mwalimu fundi wa maisha wa Taifa la Tanzania na Africa kwa sasa "Makuskill" aka Magufuli huwa hachoki kutusitizia watanzania kwa kauli yake ya kujiamini kabisa ya "jamani watanzania tunaweza,tunaweza kabisa" Na ninaimani Simba itaweza na waendelee na morali hiyo yakuwa wanaweza na ikiwezekana waizidishe na hapana watafika mbali kwani ukiangalia kitakwimu Simba kwa sasa ina safu ya ushambuliaji ilio na uwezo mkubwa hata kuliko mabingwa wa tetezi wa kombe hilo kwa sasa.

    ReplyDelete
  2. Ndoto za mchana plus sizitaki mbichi hizi.

    ReplyDelete
  3. Tulimsikia Manara akijinadi kuwa hawatafanya makosa kama yaliyojitokeza na Green Worriors, kila timu watakayocheza nayo watachukulia kama fainali na wamekuwa wakiwakumbusha wachezaji wao kuhusu hilo na wamejielewa, list ya Simba almost ileile Dida, Kungubali, Kwasi, Juurko, paul Mzamiru, Ndemla, Kichuya, Kotei, Chama, Salamba, Rashid wote wamesajiliwa, wanafundishwa na kocha mmoja. Kwa nini inaaminika kuwa ni kikosi cha pili? Ktk hali hii toundoe dhana kuwa Simba ina kikosi kipana cha kucheza muda mmoja viwanja tofauti. sasa kimewakuta tena na timu ndg. Mnaongea sana

    ReplyDelete
  4. Simba ipi ina forward kali kushinda mabingwa watetezi wa Club CL ya Afrika hawahawa kina Bocco,Kagere na Okwi.

    ReplyDelete
  5. Huyo apelekwe milembe .Na walipofungwa na Green Worriers hawakuwa na malengo? Walipofungwa na Mbao hawakuwa na malengo? Akapimwe Milembe huyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic