December 28, 2018


Droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inafanyika leo jijini Cairo, Misri ambapo jumla ya timu 16 zitakuwa zinasubiria kujua zinapangwa na wapinzani wapi.

Katika upangwaji wa makundi hayo, Tanzania inawakilishwa na klabu ya Simba iliyofuzu kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia.

Hapa nchini, wadau, mashabiki na wapenzi wa mchezo wa soka kwa ujumla wanasubiria kuweza kujua Simba itapangwa na timu zipi tayari kusubiria michezo hiyo katikati mwa mwezi Januari 2019.

Moja ya timu ambazo zipo kwenye hatua hiyo ni TP Mazembe ya DRC Congo, Al Ahly ya Misri, As Vita kutoka Congo, Orlando Pitares ya Afrika Kusini na zingine.

Tayari mwakilishi ambaye ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Sued Nkwambi ameshawasili jijini Cairo kusubiria upangwaji wa makndi hayo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic