SIMBA WATAJA KIKOSI KITAKACHOENDA MAPINDUZI CUP
Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba umepanga kukipelekea kikosi cha vijana (U20) visiwani Zanzibar kwa ajili ya mechi za Mapinduzi CUP.
Maamuzi hayo yanakuja kutokana na uwepo wa mashindano mengi ambayo Simba inakabiliwa nayo hivi sasa.
Katika mwezi Januari Simba itakuwa inakabiliana na mashindano ya SportPesa Super CUP, Ligi ya Mabingwa Afrika, Mapinduzi CUP na Ligi Kuu Bara.
Kwa taarifa za ndani kutoka Simba zinasema kuna uwezekano mkubwa kikosi cha vijana hao na ambao wamekuwa hawapati nafasi wataelekea Zanzibar.
Simba hivi sasa ipo katika mikakati ya kujipamba kuelekea mechi za hatua ya makundi ambapo imepangwa kundi D ambalo lina vigogo kama Al Ahly na AS Vita ya Congo.








Tarehe 11 au 12 January Simba watamkaribiaha Thomas Ulimwengu na warabu wake.
ReplyDeleteTarehe 18au 19 January wanatakiwa kuwepo Congo kwa As Vita. Na wakitoka Congo wanatakiwa kuwa tayari kwa safari ya Misri. Sasa hapo utaona kwa jinsi gani ratiba inavyo wabana Simba .
SAWA KABISA KUWAACHIA VIJANA WAKAPATE UZOEFU ZANZIBAR
ReplyDeleteHii inaonyesha Ni namna gani tusivyokuwa na mipango na kalenda ya msimu. Waandaaji wa mashindano Kama Sportpesa wanatakiwa kutafuta muda mwafaka, mashindano ya kombe la mapinduzi yapo kisiasa zaidi kuliko ufundi.
ReplyDeleteKikosi kipana kiko wapi? Au ndo Mashujaa wamawaumbua na kikao kipana!?
ReplyDeletetulia dawa ikiuingie
DeleteHaahahahahah
DeleteKikosi kiko wap sasa
ReplyDelete